Header Ads Widget

Responsive Advertisement

LIKE FATHER LIKE SON



SIMULIZI FUPI - LIKE FATHER LIKE SON


Nakumbuka Siku hiyo nilipigiwa simu na Sheila rafiki wa karibu wa Paris. Siku hiyo aliongea jambo tofauti kidogo na siku nyingne akinipigia simu.Kwa kifupi aliniambia naitajika kwa akina Paris na ni Paris mwenyewe ndiye aliomba niende kwao.

Paris alikuwa ni mpenzi wangu miaka nane iliyopita,lakini aliniacha bila kunipa sababu yoyote ya kuniacha.

Alianza vituko tu! Mara kanitusi,mara kanidharau na vitu vingi vya namna hiyo. Baadaye alipoona sibadili maamuzi yangu ya kumuacha aliamua ye mwenyewe kuniacha. Kiukweli niliumia lakini maisha yaliendelea na leo baada ya miaka nane naambiwa naitajika kwao na nilisisitiziwa kwenda.


*************

Japo ilipita miaka mingi bila mawasiliano na Paris lakini bado nilikua natamani nikutane naye aniambie sababu ya kuniacha, na kitendo cha kuniita kwao ilikuwa ni bahati tosha kujua ukweli huo.

Zikapita siku na siku na hatimaye siku ya kwenda kwa akina Paris ikawadia. Sikua na papara yoyote mtoto wa watu.

Kwenye mida ya saa nane mchana nikawa nipo sebuleni kwa akina Paris uso kwa uso na Mzee Ganga,baba yake na Paris..

Sikuwahi kukutana na Mzee Ganga hapo kabla,lakini Paris aliwahi kuniambia kuwa baba yake ni Mwanajeshi.

Aisee yale macho ya Mzee Ganga ni heri uangaliwe na Simba. Nilipojaribu kuyakwepa kwa kuangalia pembeni hapo macho yangu yakatua kwenye sofa fulani la mtu mmoja.Hapo nikamuona Sheila akibofya simu yake.

Nilipoangalia lile sofa la watu wengi nikakutana na sura za wanaume wanne wakiwa katika mavazi ya Kiofisini zaidi,yaani wamevalia suti na wengine mavazi ya ghalama ya kiofisini.

Nikatabasamu halafu nikajiangalia mwenyewe nilivyokuwa tofauti kimavazi na wale jamaa. Juu nilikuwa na fulana ya kahawia,chini na jeans ya bluu na mlangoni nimevua "converse" nyeusi.

Nikajisemea moyoni mwenyewe,

"Halali mzee anitazame hivi". Ghafla nikakatwa mshangao wangu kwa sauti kali kutoka kwa Mzee Ginga ikiwaita Paris na Mama yake.

Hapo nikakaa kitako,macho mlangoni kumlaki Paris wangu.

"Ee bwana ee, kumbe ile t.shirt anayo hadi leo?". Swali lilipita kichwani baada ya kumuona Paris kaja huku kavaa fulana niliyompa miaka ile niliyokuwa naye katika mahusiano.

Alikuwa hajabadilika sana, sema alikuwa kaiva sana usoni si mnajua “HOME SWEET HOME” bwana.

"Haya we Paris watu wako hawa hapa,anza mmoja baada ya mwingine,lakini anza na huyu mhuni". Mzee Ganga alimpa uwanja Paris huku akimwambia aanze na mimi...

Paris aliniangalia usoni na hapo akakutana na tabasamu moja hivi ambalo niliwahi kumuambia maana yake.Alipoliona na yeye akatasam vilevile halafu akaongea maneno fulani ya kunong'oneza,yaani yale ya kupepesa mdomo bila kutoa sauti. Hakuna aliyeelewa zaidi yangu, alisema " PLASTIC SMILE" ilo ndio tabasam tulilolitoa pale,yaani tabasam la kuzugia au la kuchonga..

"Huyu anaitwa Frank Masai.Huyu nilimpata miaka nane iliyopita na nilidumu naye kwa mwaka mmoja.

Kiukweli alinipenda sana lakini mimi ndiye nilimsaliti na kuwafata wale palee {huku anawanyooshea kidole majamaa mawili katika lile sofa la watu wengi}.Baadaye nilipata mimba ambayo nilijifungua huyo mtoto ambaye japo ana miaka saba ila hajui kuongea,kutembea bali kutoa maudenda"

Hapo Paris akataka kuacha kuongea na kutaka kuanza kulia.

Nyie acheni tu! kuna familia zinaenda kijeshi jeshi kama jeshini kweli.Baba Paris alioona Paris anataka kuanza kujiliza,alikuja juu kama kasikia mabom mlangoni kwake.

"Wewe acha ujinga wako hapa.Unataka kuanza kumlilia nani mbwa wee.

Kama alikupenda mbona ulimsaliti?Ndiyo maana mjukuu wangu ni taira.Endelea hapa hadi umalize na hichi kihuni chako kinaleta Ubongo fleva nyumbani kwangu leo ndio kitaona.

Eti tisheti limeandikwa Kanye Kanyele, ndiyo nini sasa".Aliongea Mzee Ganga huku madongo kibao yanakuja kwangu.

“Baba Paris.Embu muache mtoto aendelee kuongea.Mbona unataka kuanzisha mada nyingine tena mbele ya wageni?”.Mama Paris ilimbidi amsihi mme wake.

“Hapa hakuna nini wala nini.Hawa mabongo fleva wake lazima watambue hii ni mahakama kwa ajili yao,Pumbavu zao,na leo ha………..”.

Paris alikata yale madongo kwa kuendelea na utambulisho wake

"Nilipopata mimba ikabidi nianze kutafuta njia za kumuacha Frank. Frank alikuwa hawezi kutunza ile mimba sababu alikuwa bado anasoma na anawategemea wazazi wake,ningempa mzigo wakati nilikuwa sina uhakika kama ile mimba ni yake.

Nikamuacha Frank hivyo hivyo japo aliikuwa ananipenda sana".

Paris akamaliza upande wangu na kuwaangalia wale wageni wengine.Kisha akaendelea na utambulisho wake.

"Huyu hapo anaitwa Gasper Jonah.Huyu ndiye yule alienipaga mimba mara ya kwanza lakini aliikataa na ndiyo sababu ya ile mimba kuharibika kwani presha niliyoipataga ikasababisha mishipa ya uzazi kulegea na kufanya mtoto wangu kutoka kabla ya siku.

Mimba ilipotoka nikaamua kumsahau kwa kukutana na Frank. Lakini Frank alikuwa hana dira yaani bado alikua anawaza kusoma zaidi wakati mimi nataka kuanzisha familia. Hapo ndipo huyu Gasper akaniahidi kuwa ataniposa na mimi sikujali ya mwaka wa nyuma,nikamrudia.

Na huyo hapo pembeni yake anaitwa Josaya Sala.Huyu naye ni mvulana alinitoa usichana wangu.Niliachanaga naye muda sana lakini wakati yupo St.Augustin aliniomba turudiane na aliahidi kuja kujitambulisha nyumbani.

Nilikubali kwa sababu nilihitaji sana kuwa na familia na wakati wote huo bado nilikua na Frank huku namdanganya. Nilipopata mimba nikajua labda ni ya Gasper au ya Josaya na wote walikubali kuilea lakini hakuna aliyejua kuwa nawachezea bila wao kujuana.Mtoto alipotoka ndiyo wakajua mchezo wangu kuwa nawachanganya,na kwa sababu hiyo wote waliniacha".

Yaliongelewa mengi sana siku ile lakini mengi yalikuwa kama yananiumiza mimi.

Maneno hayo mengi yakanifanya kutoka nje na kwenda sehemu fulani hivi humo humo kwao.Kulikuwa kuna kiwanja cha Mpira wa Kikapu.

Nilimkuta yule mtoto wa Paris kajiinamia tu!. Hachezi mwili,vidole wala kupepesa macho yaani kama roboti ambalo halina betri au umeme. Kiukweli mtoto wa Paris alikua anasiktisha sana pale alipokuwa amekaa.

Huruma ilinijaa,kisha nikangalia kwenye ule mlango wa sebule niliotokea, nikakumbuka nlichokifanya mle ndani muda mchache uliopita..

Paris alipokuwa anaendelea kutambulisha alifika hadi kwa yule jamaa wa nne. Eti akasema yule alikuwa anamtaka toka zamani ndio maana akamuachia mwili wake.

Iliniuma sana ile na kuamua kutoka,lakini kabla sijatoka Mzee Ganga alibwata kwa madongo yake na hapo na mimi nikaamua kujibu mapigo,

"We mzee hatujaitwa hapa kusikiliza dhambi za mwanao wala sijaja kusikia uchafu wa mdomo wako.Nimekuja mwenyewe na niache niondoke". Nilimjibu hivyo Mzee Ganga na kutoka nje na ndipo nilipokutana na mtoto wa Paris amekaa kwenye kiti kama bembea pale nje huku kainama na mikono yake kaikunja huku shati lake likilowana na udenda..

Nilisogea hadi pale na kutaka kumshika,lakini nilisikia sauti kali ikitokea nyuma yangu,

"We we we wee, ukimgusa huyo,akianza kulia utambembeleza hadi anyamaze ata kwa masaa 10. Huyo anaguswa na mama yake tu!,Na usipomuweka hapo siku hiyo mtakesha mnamfuta machozi". Yalikuwa maneno ya dogo mmoja aitwaye Solo.

Solo alikuwa ni mtoto wa mwisho Mzee Ginga na miaka nane iliyopita niliwahi kuongea naye kwa kupitia simu ya Paris akiwa na miaka mitano na nilimuahidi nitamletea Play Station pamoja na mpira wa kikapu. Nilipomuona na kumjua jina lake nilitabasamu na kumuuliza kama ananikumbuka, alinijibu kwa kusema hapana. Hapo nilimkumbusha na alikumbuka kweli. Nilimchukua hadi kwenye gari langu aina ya Range na kufungua mlango wa nyuma na kutoa begi ambalo lilikuwa na zawadi za Solo.. Alifurahi sana kuona mpira ule na hapo akaanza kwenda nao hadi kwenye kiwanja chao na kuanza kucheza. Kwakuwa nilikuwa naweza kucheza mchezo ule,basi ikawa raha kwetu....Baada ya muda nilimuuliza Solo jina la mtoto wa Paris na aliniambia anaitwa Luther,hapo pia nilitabasamu kwani niliwahi kumpa mdoli Paris ambaye tulimuita Luther.Nilimfuata Luther na kuanza kumpa mpira ule."We Shem shauri yako,huyo ni Ambulance". Aliongea Solo kwa kunionya,lakini mimi sikukoma na nikazidi kumpa ule mpira kwa utani mwingi. Alikua kafa ganzi tu! Achezi wala kushtuka... Nilikata tamaa na kuanza kurudi nyuma,lakini wakati narudi niliona vidole vya Luther vikitikisika,hapo nilimgeukia Solo na kumwambia aje aone kuwa Luther katikisika vidole...


"Wee shem nawe,ulivyomng’ang’ania huyo kama sijui nini? Uyo hata ufanye nini atikisiki wala hachezi chezi. Mi naona unajisumbua na kunigasi,we njoo huku nikupe midunk kama ya Kobe” (Kobe ni mcheza kikapu wa Marekani,anaitwa Kobe Bryant).Aliongea hayo Solo huku akionesha kukasirika na mambo yangu nayomfanyia Luther. Niliona labda kweli ni mawazo tu! Na kujipa moyo kuwa Luther hakucheza vidole vyake hivyo nilimpa mgongo na kuanza kwenda alipo Solo....
"DADY" Nilisikia sauti hiyo nene kidogo na ya kitoto kutoka nyuma yangu wakati naenda kwa Solo. Sikutaka kufatilia sana kwani nilihisi ni mawazo yangu tu!.Nilizidi kwenda kwa Solo,lakini ilisikika sauti nyingine tena muda ule ilikuwa ya nguvu zaidi hadi Solo naye ikamfikia,"Dadie,I want to play a ball with you" {baba nataka kucheza mpira na wewe}.Ilikuwa ni sauti ya Luther ambayo iliniacha kinywa wazi huku ikimfanya Solo akimbilie ndani kwa fujo huku akimuita baba na mama yake waje washuhudie kinachotokea nje.
Wazazi pamoja na watu wote mle ndani walitoka nje kuja kuona maajabu hayo ambayo walikuwa wakiambiwa na Solo. Walipotoka walikuta nimeshika kichwa nisijue cha kufanya..Luther alikua anaweza kuudundisha ule mpira wa kikapu kama tulivyokuwa tunaweza kufanya sisi.Pia alikuwa anauwezo hata wa kufunga.Kama angepakuwa na umri mkubwa na kuongezeka urefu,angekuwa na uwezo sana kwenye mpira ule wa kikapu.Kifupi Luther alikuwa ana kipaji cha hali ya juu kwenye mpira wa kikapu licha ya umri wake wa miaka saba.Nilipogeuka kuwaangalia wazazi wa Paris na wale wageni niliona nao wakiwa katika mshangao kama wangu. Nilimuita Luther na hapo alikuja kwangu na kunikumbatia kwa nguvu na kisha akaniambia,"I love you Dady{nakupenda baba}”.Ndiyo maneno aliyotoa Luther baada ya kunikumbatia.


Alinikumbatia kwa nguvu pale kifuani kwangu kana kwamba alihisi nitamuacha endapo atanikumbatia kidogo.. Bado nilikuwa katika mshangao wa hali ya juu pamoja na maswali kedekede.Kwa nini Luther aliniita baba? Kwa nini Luther alijifanya taira? Hichi kipaji cha kucheza mpira wa kikapu katoa wapi? Na hii lugha ya Kiingereza kaijua wapi?Kichwani maswali yakajaa Luther tu!.
Nilipotupa macho kwa wakina Paris na wageni wake nikaona nao bado wapo katika mshangao ule ule.Ikabidi hivyo hivyo nitupie swali kwa wazazi wa Paris na Paris mwenyewe.
"Hivi huyu mtoto mmewahi labda kumpeleka 'international school' au labda mmewahi kumpeleka Marekani hivi ili akapate tiba matokeo yake akakutana na wacheza kikapu,wakamfundisha kikapu na lugha.Embu kuweni wazi kidogo maana dah! Nashndwa kuelewa, hadi naitwa baba". Yalikua maneno yangu ambayo niliyatoa lakini nlijua kabisa hayana majibu ya ndiyo hata kidogo."Frank, nashndiwa kuelezea kinachotokea hapo, yaani,aaah". Paris alishindwa kumalizia maneno yake na bila kusita alikimbilia pale nilipo mimi na Luther na kutukumbatia huku akitoa machozi, machozi ambayo naweza kusema yalikuwa ni ya furaha na bila kutegemea nilisikia Paris akisema,"Nakupenda Frank. Nilikuahidi wewe ndiye utakuwa baba wa watoto wangu, nimetimiza hilo". Kidogo nikapata mwanga kuwa kumbe Paris anajua nini kinaendelea. Maswali yakabaki juu ya lugha na kipaji chake lakini kabla sijaendelea likajitokeza suala lingine..
"Baba lile si ndio gari lako eeh!. Range Rover ya mwaka 2010, injini yake ni silva ambayo si rahisi kushika kutu, na pia lina uwezo wa kwenda kilometa zaid ya 450 kwa mwendo kasi uleule na bila kupumzika.Pia zile gari zenyewe kabsa kutoka Uingereza huwekewa nakshi za almasi katika tairi zake au ndani ya gari,lakini najua lako halina." Yalikuwa maneno ya Luther ambayo sasa niliyachoka ikabidi nimuulize yeye mwenyewe.
"Wewe Luther haya yote umeyajuaje?"


"Baba najua huwezi kuamini,lakini najua mengi kuhusu haya maisha yetu. Kitendo cha mimi kujifanya taira ni kutaka kuwaonesha kuwa mambo wanayofanya siyo mazuri. Babu alimfukuza mama kisa tumbo lake alilokuwa kanibeba mimi.Huko tulipoenda ikawa ni vurugu kila kukicha.Baada ya kuzaliwa sasa ndio mambo yakawa mambo, nikakosa malezi muhimu kabisa. Hao mama aliyosema ni baba zangu,wote walimkana sababu aliwachanganya. Nakupenda sana Baba,ningesipo kuona ningekuwa taira daima. Kitendo cha wewe kuja na mpira pale uwanjani niliipata harufu yako na kujua wewe ndiye baba yangu..Baba, wewe wajua kucheza mpira wa kikapu pamoja na uncle Solo,basi kaa ukijua nimerithi kwanu sema mi Mungu kanipa nikiwa mdogo, ni mengi nimebeba kutoka kwako kama usanii wa kuchora na utunzi.Kuhusu mimi kujua haya magari na mambo kama kompyuta hayo nimechukuwa kwa Babu, nadhani atakuwa anaelewa. Baba, naomba uondoke na mimi tukaishi pamoja". Alimaliza Luther huku akifuta mafua ambayo nadhani yalikuja sababu ya kutaka kulia.


Hapo ndipo nikaamini dunia ina mengi na Mungu ni wa ajabu pia.Luther alikuwa wa kutokwa udenda kutwa nzima, Luther alikuwa hatikisiki wala kuongea, leo hii mtoto anapiga kikapu kama Kobe Bryant. Mtoto ana mambo kama ya Bill Gates na anaongea kama kafungwa radio au memori kadi. Na kumbe muda wote huo wa miaka saba alikuwa anajifanyisha au sijui labda MUNGU alimfanya vile hadi siku nitakapotokea.Nikatabasamu halafu nikarudi kimawazo hadi utotoni kwangu.Nilikuwa kama sitaki kitu basi siku hiyo nitakuwa bubu hadi nitimiziwe.Nikacheka zaidi na kusema,kweli hii ni "LIKE A FATHER, LIKE A SON"{kama baba, kama mwana}au kwa kiswahili elevu ni sawa na kusema,"Ni kama baba yake huyu mwana". Maneno ambayo yalimfanya Luther acheke na kusema,"We ndiye baba yangu"*************Walikubali niende kuishi na Luther baada ya kupima DNA na kugundulika kuwa alikua ni mtoto wangu kweli..Paris yeye aliolewa na Gasper japo aliniambia kuwa angefurahi kuwa na mimi,lakini mimi nilimwambia sipo tayari huku nikikumbuka mambo aliyonifanyia Paris huko nyuma.Huyo aliyemuoa,sikujali yatakayomkuta na wala sikutilia maanani.Maisha yangu rasmi yakaanza mimi na Luther Genius.
MWISHO

Post a Comment

0 Comments