Header Ads Widget

Responsive Advertisement

KULA NILIKULA LAKINI SIKUSHIBA



SIMULIZI FUPI - KULA NILIKULA LAKINI SIKUSHIBA


“Nyamaza basi kaka …mbona hivyo….. unalia kama mtoto mdogo wakati wewe ni mtu mzima?” “Wacha nilie mimi ihiiiii unazani yaliyonikuta ni madogo?” “Hata kama si madogo lakini si ujikaze kama mwanaume?” “Wewe unasema hivyo kwa sababu hayajakukuta.” Kwani kuna nini kimekukuta?” “Ahaaaah inauma ,,,,,,,,inauma sana,,,,,, wacha kwanza nilie nipoze machungu.”

Baraka alikuwa akilia huku akibembelezwa na jamaa aliyemuona akilia.Jamaa huyo alimchukua Baraka mpaka sehemu yenye viti na kukaa na kumsihi Baraka anyamaze na amweleze ni nini kilichomsibu.Ndipo Baraka alinyamaza na kumsimulia. “Muuza fruits wangu jamani, sitomuona tena mimi.”

“Mwaka 2007 nikiwa masomoni hapa mkoani Mbeya katika chuo kikuu cha Mzumbe, nilimuona binti mmoja akiuza matunda mle chuoni cafeteria.Alikuwa ni mzuri sana, mwenye shepu ya kinyakyusa, aliitwa Diana, mweusi wa kuvutia,mwenye chuchu ndogo ,urefu wa kati ,mwili umejaa jaa kiasi cha kutamanisha.Nilikuwa si mpenzi wa kula fruits lakini nilipomuona yule binti nikawa naenda pale kununua matunda yake huku nikiwa namsabahi na kuanza kujenga nae mazoea.Kila nilipokuwa naongea nae tulikuwa tunaangaliana machoni na alikuwa akiniongeza matunda zaidi ya kipimo cha kawaida.Nilifanikiwa kumweleza kuwa nimetokea kumpenda nae bila kujivunga akaniambia hata yeye alitokea kunipenda tatizo ni kuwa yeye ni darasa la saba na mimi elimu yangu ni ya chuo tutaendana kweli.Nikamwambia asijali mapenzi hayachagui ila ni upendo wa dhati baina ya jinsia mbili tofauti.

Mapenzi yetu yakaanzia hapo tatizo likaja wanachuo masharobaro wa certificate na diploma wakawa nao wanamtongoza sana lakini akanihakikishia kuwa amenipenda mimi nami nisiwe na wasiwasi nae hatonisaliti. Diana alikuwa anapata fedha nyingi kutokana na biashara yake mpaka akafungua stationary mle mle chuoni nyuma ya cafeteria karibu na recreation pub na alipata wanafunzi wengi kutokana na huduma yake kuwa nzuri na wanachuo walimpenda kutokana na ucheshi wake.

Nilipohitimu chuo nilirudi nyumbani Dar es salaam na kuanza kutafuta kazi lakini miaka miwili bila mafanikio ya kupata kazi.\Mimi na Diana muda wote huo tulikuwa tunawasiliana kwa simu na akanishauri kutokana na kutopata ajira mimi niende Mbeya nikaungane nae kufanya biashara kuliko kukaa nyumbani nikiendelea kutafuta kazi.Nilikubaliana na ushauri wake na kurudi Mbeya kufanya biashara anayoifanya pale chuoni.Nikawa ninaishi kwake alipopanga huku tukifanya kazi kwa pamoja .Kutokana na mimi kusomea masomo ya biashara nikapanga mikakati ya kuifanya biashara ya Diana kuwa kubwa zaidi na kuiendesha kisomi na kweli ndani ya muda wa miezi nane biashara ilikuwa sana na kila mwanachuo aliijua ofisi yetu hata wanachuo kutoka vyuo vingine walikuja kwetu kupatiwa huduma.

Baada ya miaka miwili nilipata barua kutoka uongozi wa chuo ukinitaka nifanye kazi nao kwa maana mimi ni mwanafunzi wao na vile vile wameona matokeo ya biashaya yetu inavyokuwa kwa kasi na hata alama zangu za matokeo nilikuwa na gpa ya 4.3 hivyo nikapewa ajira kama mhadhiri msaidizi huku nikisomeshwa shahada ya pili bure hapo hapo chuoni.Nilifurahi sana kupata ile barua ya wito hata Diana nae nilipomwambia alilia machozi ya furaha na kumshukuru mungu.Nikaanza kazi pamoja na kusoma shahada ya pili na nikiendelea kusimamia biashara zetu na baada ya miaka mitatu nikawa nimeshajenga nyumba,nimenunua magari mawili,nikamuoa Diana rasmi na kuipanua zaidi biashara yetu.

Ghafla baada ya mwaka mmoja mbele nikabadilika, nikawa mtu wa starehe starehe na mimi,nabadilisha wanachuo wa kike kama nguo,nyunbani silali,pombe na mimi mimi na pombe.Diana alishangaa kubadilika kwangu ,akiniuliza tu nilimpiga mpaka akawa anapoteza fahamu na huku akiwa na mimba ya miezi minne.Biashara yetu ikaanza kudolora kutokana na mimi kutozingatia tena biashara na Diana ujauzito ulikuwa unamsumbua,ikafika kipindi biashara ikafungwa.Diana akawa mtu wa kukaa nyumbani akilea ujauzito wake,mimi nikawa na kwenda na wanawake zangu mpaka nyumbani,Diana akawa analia sana na akilalamika tu namshushia kipigo bila kujali mimba yake.Kutokana na kuendekeza starehe na pombe nikajikuta nashindwa hata kufundisha,uongozi wa chuo ulipoona hivyo ukashindwa kunivumilia kwani Diana alishanilalamikia sana kwa mkuu wa chuo na nilionywa mara nyingi lakini sikubadilika na mwishowe wakanifukuza kazi.

Baada ya kufukuzwa kazi maisha yakaanza kuwa magumu nikaamua kuuza magari yote mawili huku nikiendelea kuponda raha na mabinti wadogo wadogo.Baada ya muda mchache fedha zikaisha nikaamua kuuza nyumba,Diana nilimfukuza arudi kwao mimi niendelee kula starehe.Fedha nilizopata kwa kuuza nyumba niliibiwa siku ile ile ya kwanza kwani nilimchukua changudoa pale carnival mafiati usiku.Nikabaki sina kitu mfukoni ,kutokana na nilikuwa naishi hotelini muda wa kukimiliki chumba ulipoisha nikafukuzwa hotelini.Nikawa mtu wa kuwafuata marafiki zangu na kuwaomba hela lakini walipochoka kunipa wakawa wananikimbia.

Maisha yakawa magumu kupitiliza nikawa mtu wa kuzurula mitaani na kulala nje.Miaka miwili nikawa naishi hivyo kama chizi.Siku moja usiku saa saba nikiwa nimelala katika uwanja wa mpira wa shule ya sekondari sangu nilishangaa napigwa na radi huku kukiwa hakuna mvua na mara nikawa navuta kuinuliwa juu kwenda angani.Niliinuliwa kwenda juu kama urefu wa ghorofa tano ndipo nikawa napelekwa kwa kuelekea Uyole kwa kasi sana kama nipo kwenye ndege .Nikawa nashangaa huku nikitetemeka kwa hofu na nilipofika katika uwanja wa mpira uliopo kati ya kwa mama John na Ilomba nikawa nashushwa kwa spidi kali na kudondokea katikati ya uwanja na kupotezafahamu.Nilirejewa na fahamu baada ya nusu saa ndipo nilipowaona watu wanaomba na kukemea kwa jina la yesu, nikajihisi hali ya mabadiliko kiakili na kimwili nikabaki najishangaa na nawashangaa hao watu.


Waliendelea kuomba mpaka saa nane na nusu nilistuka kumuona fisi akitokea barabarani akija kwa kasi sana kunielekea mimi huku akiunguruma.Niliogopa sana na alipokaribia kunifikia nilishangaa amebadilika na kuwa mtu tena mwanamke na hapo hapo akadondoka chini na kupoteza fahamu.Wanamaombi wale waliendelea kuomba mpaka ilipotimia saa tisa ndipo walipomaliza na kutukuta mimi na yule mwanamke tuko pale chini.Walitusogelea na mmoja ambaye ni mchungaji aliwaamuru baadhi wanichukue mimi na kunikalisha kwenye kiti na Yule mwanamke baadhi wakampatia huduma ya kwanza na baada ya dakika chache akalejewa na fahamu na kukalishwa kwenye kiti.Nikawa nawashangaa na kuwauliza mbona niko hivi ,wakaniambia nilikuwa nimechanganyikiwa akili kwa kurogwa .Nilistuka sana na wakaniambia alieniloga ni huyo mwanamke.Mwanamke Yule alikuwa akilia na kusema,,,,”Nimekosa jamani nahitaji msamaha wenu na wa mungu pia.Baraka

 mimi kiasilia ni mchawi mkubwa tu hapa Mbeya,niliamua kukoroga wewe baada ya wewe na mkeo kuzidi kuliteka soko lote la huduma ya stationary pale chuoni na wanachuo wakawa hawatoki nje ya chuo kufuata huduma zetu bali wanaudumiwa na nyinyi huko huko ndani.Na niliposikia kuwa umeajiliwa na chuo kuwa mhadhiri msaidizi roho yangu iliniuma sana,nikaapa lazima nikuroge.Nilichagua kukuloga wewe badala ya mkeo kutokana na kuwa wewe ndiye uliyeleta mafanikio makubwa katika biashara za mkeo hivyo nilipoamua kukuroga wewe nikajua kabisa mkeo hatoweza kuendesha biashara bila wewe hivyo angeshindwa na kufunga biashara na hivyo ndivyo ilivyokuwa.Nilikutupia mapepo machafu ya kupenda sana ngono ,pombe na starehe muda wote mpaka ukashindwa kusimamia biashara na kufanya kazi ya kufundisha na mwishowe ukafukuzwa kazi.Ulipoishiwa fedha za kufanya starehe ukauza magari na nyumba na kumfukuza mkeo arudi kwao na wewe ukaamia hotelini,hiyo haikuwa akili yako bali ni mimi ndiye nilikuwa naichezea akili yako kiulozi na ndipo ukaibiwa fedha ila si kweli yule changudoa alikuibia zile fedha bali ni mimi niliziiba kichawi na wewe ukajua ni yule changudoa na baada ya wewe kufukuzwa hotelini ukawa mtu wa kuombaomba na mwishowe nikakutia uchizi kabisa ukawa mtu wa kuzurulazurula mchana kutwa,kula majalalani,kuo kota okota makopo,kulala mitaloni,kupiga piga watu na mawe na fimbo na kuongeaongea peke yako .”

Alisimulia yule mwanamke huku akilia sana.Ndipo na mimi nikamkubuka kumbe ni mama Mariam anayemiliki nae biashara kama yetu ya stationary nje ya chuo kule kwenye soko la maghorofani karibu na chuo kikuu huria cha Tanzania(Open university of Tanzania) na nyuma ya kituo cha kuuza mafuta cha Total.Roho yangu iliniuma sana ,huyu mama tulikuwa tunamsaidia sana matatizo yake pale kipindi vifaa vyake vilipokuwa vimearibika tulimwazima vya kwetu na pesa muda mwingine tulimpa kipindi biashara yake inapokuwa si nzuri na sisi tulimchukulia kama mama yetu,looh kumbe ni mchawi na ndiye aliyeyaharibu maisha yangu.Niliinuka kwa hasira nikitaka nimpige lakini wanamaombi na mchungaji waliniwahi na kunituliza.

***********

Mara katika lile kundi la wanamaombi nilimwona mwanamke mmoja akiwa analia sana,wanamaombi wengine wanawake wakawa wanambembeleza na muda huo huo mwanamaombi huyo akadondoka chini na kupoteza fahamu.Wanamaombi wakaanza kumpatia huduma ya kwanza lakini kila walipo jaribu wakashindwa ndipo mchungaji akatoa wazo wampeleke hospitali ya mkoa akapewe matibabu.Wanamaombi kadhaa wakapanda gari iliyokuwepo hapo uwanjani na kumuwahisha hospitali yule mwanamaombi mwenzao.Pale uwanjani tulibaki mimi na mchungaji pamoja na wanamaombi wengine ndipo nilipo muuliza mchungaji mbona yule mwanamke alikuwa analia sana,akanijibu,,,,”Yule ndie mkeo alikuja hapa jana katika mkutano wa injili unaofanyika uwanja huu kuanzia saa tisa jioni mpaka saa kumi na mbili.Baada ya mkutano alinitafuta na kunieleza mkasa uliokukuta .Nilimwonea huruma sana ndipo nikawaomba wanamombi wengine waende majumbani mwao wakapate chakula halafu saa nne usiku warudi tufanya maombi ya kukukomboa wewe katika nguvu za kichawi .Ndipo saa tano kamili usiku tukaanza maombi na ndio hayo unayoyaona yametokea muda uliopita kwani ulivutwa na nguvu za maombi kutoka huko ulikokuwa na kuletwa hapa .

Hivyo hivyo kwa mbaya wako aliekuroga nae alivutwa na nguvu za maombi yetu na kuja hapa.”Dah nilistuka sana kumbe yule mwanamkea aliyekua analia ni mke wangu nilikuwa nimemsahau kabisa,palepale nikamtaka mchungaji twende huko huko hospitali nikamuone mke wangu ,lakini mchungaji akakataa akasema tungoje mpaka asubuhi kwani kwa jinsi nilivyo mchafu natakiwa nioge kwanza na kubadilisha nguo.Nilioga pale pale uwanjani katika vyoo vya muda vilivyojengwa na nikaletewa nguo mpya asubuhi na kubadilisha .Yule mwanamke mchawi alikabidhiwa kwa viongozi wengine wa mkutano ule kwani asinge weza kukimbia kutokan na kuharibiwa nguvu zake za kichawi na maombi.Saa mbili asubuhi tukawa ndani ya hospitali ya mkoa wa Mbeya iliyopo eneo la magorofani na tuliwakuta wanamaombi wengi wapo hapo.Ndipo daktari alituita mimi na mchungaji ofisini kwake.”Hali ya mgonjwa wenu si nzuri,kutokana na kulia sana amesababisha mshipa mmoja wa damu kupasuka kichwani mwake…….”Kabla hata daktari ajamaliza kutueleza hali ya mke wangu nilijikuta nimeinuka kitini na kutoka nje mbio mbio mpaka nyuma ya hospitali na kuanza kulia.

Nililia sana kuona mke wangu atapasuliwa kichwa ili azibwe mshipa wa damu uliopasuka.Mawazo yalinijia kuwa mke wangu atakua amefariki ila daktari anaficha.”Baraka alimsimulia yule jamaa. “Dah pole sana ndugu,ila yote ni maisha tu yakupasa kuwa imara na umwombe mungu amponye mkeo.”Yule alimwambia Baraka. Muda huo huo kundi la wanamaombi wakiongoza na daktari pamoja na mchungaji linawafikia.”Aise tumekutafuta sana ,tumezunguka hospitali yote lakini hatujakuona,tukazani labda umekwenda kujinyonga ndipo daktari akatushauri tuje kukuangalia huku.”Alisema mchungaji.Baraka akabaki akiwaangalia ndipo yule jamaa akasema.”Nipo nae hapa ,nilimkuta kule akiwa analia sana nami nikamuonea huruma na kumsihi anyamaze na ndipo nikamleta hapa na kuanza kuniadithia mkasa uliomkuta.” “Tunashukuru sana ndugu kwa msaada wako mana kama kusingekuwa na mtu anayemuangalia angeweza hata kujizuru.”Alisema mchungaji. “Baraka usipaniki ,mkeo anaendelea vizuri na tayari ameshafanyiwa upasuaji na amelazwa kule wodi ya wagonjwa mahututi kwa ajili ya uangalizi wa karibu zaidi.Tunasubiri akilejewa na fahamu tutamuamishia wodi ya kawaida na mtakwenda kumuona.”Alisema daktari.

Wanamaombi walimchukua Baraka na kurudi nae nyumbani kwa mchungaji na jioni ilipofika walikwenda hospitali na kumkuta mkewe amerejewa na fahamu na kuamishiwa wodi ya kawaida ya wanawake lakini hakuweza kuongea chochote ingawa anaona. Maisha ya Baraka yakaamia kwa mchungaji na baada ya mwezi mmoja mkewe akaruhusiwa kutoka hospitali na kuungana na mumewe nyumbani kwa mchungaji.

Kutokana na wazazi wa mkewe kufariki mwaka mmoja uliopita katika ajali ya basi wakiwa wanatoka Tukuyu kuja Mbeya mjini,nyumbani kwao Diana alibaki yeye peke yake na mtoto aliezaa baada ya kufukuwa na Baraka alichukuliwa na dada yake anayeishi Chunya hivyo Diana kumtaka Baraka waamie kwao kwa muda halafu baadae Baraka atafute kiwanja na kujenga nyumba mpya.Baada ya Baraka kuamia ukweni kwa mkewe waliamua kumchukua mtoto wao kutoka kwa dada yake na Diana.Baraka alifurahi sana kumuona mwanae tena wa kiume amefanana naye kila kitu na kila anapomwangalia mwanae machozi yanamtoka kutokana na kumbukumbu ya maisha aliyopitia.Wazazi na ndugu wa Baraka walipewa taarifa ya Baraka kupona ,nao walifurahi sana kwani wazazi wa Baraka nao waliangaika sana kumuokoa mtoto wao lakini walishindwa na kuamua kumuachia mungu.

Baraka akawa anafanya kazi na yule mchungaji na baada ya miaka miwili Baraka nae akafungua kanisa lake na kuliita KANISA LA BARAKA ZA MUNGU .Wazazi wake walifurahi sana kusikia baraka mtoto wao kafungua kanisa ,nao wakampa fedha kidogo za ujenzi wa kanisa hilo.Baadaya miezi sita Baraka akapokea barua kutoka chuo kikuu cha mtakatifu Agustino wakimwomba awe mhadhiri kama alivyokuwa anafundisha chuo kikuu mzumbe.Kwahiyo akawa na kazi mbili ya uchungaji na uhadhiri pia na baada ya mwaka mmoja akaruhusiwa kusoma phd bure kabisa gharama zote zinalipw na chuo.Yule mwanamke mchawi aliyemloga alishindwa tena kuwa mchawi na kumrudia mungu wake na sasa anafanya kazi ya kuhubili injili katika kanisa la Baraka.Baraka baada ya miwaka miwili akahama ukweni na kujenga nyumba yake ya kisasa pamoja na kununua magari ya kutembelea.Baraka kila anapokuwa akiwaza maisha aliyopitia huwa anajisemea moyoni KULA NILIKULA (wanawake,pombe,starehe za aina mbalimbali) LAKINI SIKUSHIBA kumbe nililogwa looh.
MWISHO.

Post a Comment

0 Comments